Ndanda

CT Scan

Hosteli

Tangu miaka kadhaa, tuna mpango wa kujenga  hosteli kwa ajili ya madaktari tarajari na wafanyakazi wengine. Kutokana na eneo kuwa na soko na maduka binafsi kumekuwa na ukomo. Kwa viwango vya nyumba za kulala kwa afya, umeme na maji ni duni na wakati mwingine zimekuwa mbali  kutoka hospitali. Kwa upande mwingine idadi ya wafanyakazi kwenye taasisi yetu inaongezeka mwaka hadi mwaka. Mahitaji ya malazi kwa wafanyakazi wetu wa muda mfupi ni muhimu sana,Pamoja na wataalamu wanaotutembelea kutoka nje na  madaktari tarajari ambao wanafanyakazi mwaka mmoja.

Kwa hiyo tumeamua kujenga hosteli upande wa pili wa barabara kuu. Itakuwa na majengo kadhaa tofauti na makundi mbalimbali ya wageni. Jengo la kwanza wageni wa hospitali wanaojitolea, kama wataalamu wanaotutembelea kutoka nchi za nje. Jengo litakuwa na vyumba 10 vilivyojitosheleza, mapokezi, jiko, eneo la chakula na sehemu ya kufua nguo. Ujenzi wa jengo hili umeanza mwezi wa tano mwaka 2023 na utakamilika katika robo ya kwanza ya mwaka 2024. Katika hatua ya pili tunapanga kujenga hosteli kwa ajili ya wanafunzi wa chuo cha Ndanda COHAS.