Ndanda

Kuwafikia Watoto

Shukrani kwa msaada wa ukarimu kutoka kwa mmoja wa wafadhili wetu, tumeweza kutambua mradi huu wa kuwafikia watoto.
Daktari wetu wa watoto anatembelea mara moja kwa wiki, zahanati moja kati ya tano na kituo cha afya ndani ya wilaya ya masasi na wilaya inazoizunguka.
Wakati wa kuwatembelea watoto wanachunguzwa kwanza na daktari msaidizi wa kituo husika, na kupangiwa siku ya uchunguzi mwingine na mtaalamu wa watoto.

Kwa wastani watoto 12 hadi 15 hupatikana kwa ushauri na matibabu kila  anapowatembelea mtaalamu wa watoto wakati mwingine hufika hadi 30.
Watoto hao hupatikana na hali tofauti za kiafya kwa kutaja chache ni kama shida za moyo, magonjwa ya figo, upungufu wa damu, utapia mlo, kifafa na kasoro za kuzaliwa.
Hospitali yetu inatoa huduma bure kwa zahanati na vituo vya afya.
Wazazi wa watoto wanapaswa kulipa ada ya kituo husika ambayo inamaanisha kuonwa na daktari ni bure kwa watoto chini ya miaka mitano na kwa kuonwa na daktari umri zaidi ya miaka mitano ni Shilingi elfu tano tu.