Ndanda

Idara ya Ustawi wa Jamii

Dhumuni halisi ya Idara hii ni kuhudumia wagonjwa maskini wasioweza kujigharamia matibabu kama vile vipimo, vifaa tiba, dawa na upasuaji. Baadhi yao pia wanasaidiwa kupata chakula cha hospitali na nauli ya basi kurudi makwao.
Afisa Ustawi Wa Jamii kazi zake hasa ni kuchunguza na kubaini wagonjwa wasioweza kulipia gharama za matibabu na kisha kuwasaidia pale inapowezekana.
Sambamba na hilo anatoa huduma ya Ushauri katika masuala mbalimbali ikiwa pamoja na kutoa elimu ya sheria kutatua migogoro ya familia.

Abdulkarimu J. Kambona, 26 years old, alipatwa na ajali mbaya Mwaka 2019 Wilayani Nachingwea na kukimbiziwa Hospitalini kwetu kwa matibabu zaidi. Aliruhusiwa na kutakiwa kuja kutoa chuma baada ya miezi kadhaa.
Lakini mbaya zaidi alikuja Hospitalini mnamo tarehe 09/03/2021 akiwa mwenye hali mbaya ya mguu kutokana na kutelekezwa na ndugu zake muda mrefu. Hospitali imeokoa uhai wake kwa kumsamehe gharama za matibabu zipatazo TSH800.000/=.

Na wagonjwa 46 walipata msamaha wa muda ambao walitakiwa kurejesha pesa kidokidogo na kiasi cha TSH 13,000,000/= zimetumika. Hata hivyo jumla ya watoto 243 wenye umri chini ya miaka kumi na mbili (12) wamepata msamaha kupitia mradi wa kusaidia watoto hao. Jumla fedha za kitanzania TSH 23,000,000/= zimetumika.

Huduma katika kitengo cha ustawi wa jamii bado zinaendelea kupatikana kwa wagonjwa wa nje, ndani, jamaa za wagonjwa na kwa watumishi wa hospitali pia.