Ndanda

Sisi ni nani?

Hospitali ya rufaa ya mt. Benedicto inajulikana vizuri kusini mwa tanzania katiaka utoaji huduma bora, Hospitali hii ni ya kidini inayomilikiwa na kuongozwa na Ndanda Abbey.Dhamira yetu ni kutoa huduma bora kwa wagonjwa wote bila kujali itikadi za kidini, kichama au kiuchumi

Hospitali inawafanyakazi 320, madaktari bingwa 6, madaktari wasajiliwa 8, madaktari wasaidizi (AMO) 3, madaktari wanafunzi 20, na manesi 102. Wagonjwa hutokea maeneo mbalimbali ikiwemo Msumbiji, Dar Es Salaam hata Zanzibari. Tunajumla ya vitanda 300 kwaajili ya wagonjwa waliolazwa katika wodi 12, kwa mwaka 2019 tuliwahudumia wagonjwa wa ndani 8,248 na wagonjwa wa nje 89,608

Tunatoa huduma za kubobezi kwa kutumia mashine za kisasa, maabara yetu ina hadhi ya nyota tano vile vile tuna Xray ya kidigitali, mashine za altrasaundi za kisasa, na kipimo cha video endoscopy. Wafanyakazi wetu wanaujuzi na hutoa huduma iliyo bora kwa kila mgonjwa.

Lengo letu ni kutoa huduma bora na zakisasa kwa garama nafuu zaidi. Wagonjwa wanaohitaji hudumu za binafsi wanayo fursa ya kuchagua kulazwa katika wodi binafsi za daraja la kwanza au la pili. Garama zinazolipiwa kutoka daraja la kwanza na la pili husaidia kupooza bei ya matibabu kwa wagonjwa wanaolazwa kwenye wodi za kawaida yaani daraja la tatu.