Ndanda

Upanuzi wa Ndanda COHAS

Tangu mwaka 2019 kozi ya wataalamu wa maabara inapatikana katika chuo cha Ndanda cha Afya na sayansi shirikishi    (Ndanda COHAS)  Mipango ya programu zingine  itaanza  miaka michache ijayo. Kwa sasa tuna uhaba wa vyumba vya madarasa na vyumba vingine kwa kazi zingine. Kwa hiyo tumepanga kuongeza chuo chetu kwa kujenga jengo mpya litakalo kuwa na bwalo la chakula, maabara ya kompyuta na maktaba.

Jengo jipya limejengwa karibu na jiko la chuo. Ghorofa ya chini kuna bwalo la chakula kwa wanafunzi 220, pia kuna vyoo. Katika ghorofa ya kwanza kutakuwa na nafasi ya maktaba na maabara ya kompyuta. Vyumba vya awali ambavyo vilitumika kwa chakula, maktaba na maabara ya kompyuta vitatumika kwa madarasa. Ujenzi umeanza mwezi wa tano 2022 na utakamilika ndani ya miezi sita.