Ndanda

Mtambo wa kujaza Oksijeni

Kutokana na janga la Covid 19, mahitaji ya oksijeni yameongezeka katika hospitali nyingi, ikiwa ni pamoja na kituo chetu cha Ndanda.
Mwaka 2020 tumefanikiwa kufunga mtambo wa kuzalisha oksijeni ambayo inatumika kitengo cha wagonjwa mahututi, kitengo cha utunzaji wa watoto wachanga, uchujaji wa damu kwa wagonjwa wa figo, chumba cha uzazi na chumba cha upasuaji. Oksijeni inasafirishwa kwenda eneo husika kupitia mabomba maalum. 
Kwa uwepo wa uzalishaji oksijeni tunataka kuweka kituo cha kujaza oksijeni.

Mtambo wa kujaza oksijeni unaweza kuhifadhi oksijeni kwenye mitungi ya gesi kwa mgandamizo wa baa 100 – 150.
Mitungi ya gesi ya oksijeni inahitajika kwa usafirishaji wa wagonjwa wanaohitaji oksijeni. Kituo cha kujaza oksijeni pia kitawezesha kutoa oksijeni kwa hospitali zilizo karibu. Na mwisho lakini kwa uchache mtungi wa gesi ya oksijeni ni muhimu sana kwa akiba inapotokea kasoro ya kiufundi. Oksijeni inaweza kutumika kutoka kwenye mtungi wa gesi hadi mtambo wa uzalishaji oksijeni umerekebishwa.
Wakati tumepanga kufunga kituo cha kujaza oksieni, tunapanga kuongeza bomba la oksijeni kuelekea wodi ya watoto, idara ya wagonjwa wa nje (OPD) dharura na wodi ya daraja la kwanza.
Mkataba wa mradi huu umesainiwa mapema mwezi wa saba mwaka 2021. Kwa sababu ya ugonjwa wa Korona muda wa utengenezaji na usafirishaji  umesogezwa mbele. Tunatarajia utoaji na usanikishaji ifikapo mwezi wa kumi na moja mwaka 2021.