Ndanda

Mtambo wa kuzalisha oksijeni

Kutokana na janga la kuenea kwa virusi vya Covid 19 duniani uongozi wa hospitali umeamua kujenga mtambo utakaozalisha hewa ya oxijeni.

Mtambo wa oksijeni utazalisha hewa itakayo tumika katika kitengo cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum, watoto wachanga wanaohitaji uangalizi maalum, chumba cha upasuaji na wadi ya wazazi.hewa hii itasafirishwa kwa njia ya mabomba kutoka kwenye mitambo kwenda wodi husika.

Uwepo na upatikanaji wa oksijeni ni moja kati ya kigezo ili kuweza kufunga mashine itayo saidia wagonjwa kupumua (Artificial ventilation) katika ICU yetu.
hadi sasa kusini mwa Tanzania hakuna mashine hii, lakini tunatarajia kuwa na mashine tatu za kusaidia watu kupumua (ventilators) katika ICU yetu mpya.

Gharama za uzalishaji wa oksijeni katika mtambo huo ni shilingi 337.500.532 . Mtambo huo utakuwa na jenereta ambapo ujenzi unaendelea, gharama za jengo na jenereta ni shilingi 67,481,764 za kitanzania. Gharama kuu ya mradi wote ni shilingi 404,982,296 za kitanzania. Ujenzi wa nyumba ya jenereta na mradi kwa jumla unategemea kukamilika mwezi wa sita mwaka 2020.

Pin It on Pinterest