Ndanda

Msamaha kwa Watoto

Shukrani zetu za dhati zifike kwa Daktari bingwa wa watoto toka ujerumani, asante kwa msaada hospitali imetekeleza huduma ya ‘Msamaha kwa Watoto’

Watoto wote ambao wazazi wao wanashindwa kulipia huduma za vipimo na matibabu na kuthibitishwa na daktari wamefaidika na msaada huu.

Hadi sasa zaidi ya watoto 200 chini ya miaka 12 wamefaidika na mpango huu hususani mwezi wa Disemba 2021. Kwa mfano, watoto wenye vidonda vikubwa vilivyosababishwa na ajari ya moto ambao wanahitaji upandikizwaji wa ngozi, watoto wenye majeraha makubwa kutokana na kuumwa na mamba, watoto wachanga wanaohitaji uangalizi maalum (NICU) au watoto wenye matatizo ya figo kushindwa kufanya kazi ambao wanahitaji huduma ya uchujaji damu. Huduma ya uchujaji damu ni huduma ya kisasa na yenye gharama kubwa kutolewa kwenye taasisi yetu. Tunashukuru kwa mradi huu, hadi sasa watoto watano (5) wametibiwa kwa mafanikio makubwa kwa huduma ya uchujaji damu kwa njia ya tumbo au uchujaji damu kwa njia ya damu kwa muda wa miezi kumi na mbili (12) iliyopita.