Ndanda

Chumba cha wagonjwa mahututi na Usafishaji wa FIGO

Miradi iliyopewa kipaumbele kwa mwaka 2019/2020 ni ujenzi wa jengo la wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum,ikiwa ni pamoja na watoto wachanga (NICU) na huduma ya matibabu ya figo.

Jengo limejengwa katikati ya hospitali karibu na wodi ya kujifungulia kinamama lakini pia limepakana na jengo la upasuaji.Muunganiko huo wa huduma tatu muhimu ambazo tumezitaja hapo juu zinaleta ushirikiano katika kutoa huduma kwa wagonjwa wetu. Huduma ya wagonjwa wa figo zitapatikana ICU na wauguzi wataungana katika kutoa huduma zote tatu kwa pamoja.

Muundo wa ramani ya jengo umechorwa na International architectural office (rrp international) ikiwahusisha kandalasi waliobobea katika ujenzi wa Majengo yanayohusu tiba

Gharama ya mradi inakadiliwa kuwa shilingi milioni mia saba arobaini na sita laki saba ishirini na nne elfu, mia sita kumi na tano na sent kumi na nne (746,724,615.14) za kitanzania. Tunawashukuru wafadhiri na wahisani mbaalimbali waliojitolea kutusaidia,hadi sasa tumeshapokea shilingi milioni mia sita na tano , laki saba arobaini na moja na senti kumi za kitanzania (Euro 235000).

Ujenzi huu umeanza mwezi wa kumi mwaka 2019 na unategemewa kukamilika mwezi wa sita 2020.

Pin It on Pinterest