Faragha kwa wagonjwa wetu imepatikana kutokana na kujenga ukuta na kufunga mapanzia. Ufuatiliaji wa karibu wa wagonjwa unapatikana kupitia mfumo wa mawasiliano na sehemu maalumu ya muuguzi katika chumba, kuna vitanda viwili karibu na kituo cha wauguzi kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu zaidi. Kila kitanda kina vifaa vya kupata oksijeni, madirisha mapya yamewekwa na taa za kisasa za LED hutoa mwanga wa kutosha, chumba kimoja kimeandaliwa kwa ajili ya wagonjwa wenye maambukizo, chumba cha chai kwa waugzuzi, chumba cha daktari, ofisi ya muuguzi kiongozi, chumba cha kusafisha vifaa na stoo. Usafi umeimarishwa kwa ukarabati wa choo pia kwa matumizi ya walemavu. Ukarabati wa wodi zilizokarabatiwa unathamaniwa sana na wagonjwa pamoja na wafanyakazi wetu. Tunawashukuru sana wafadhili wetu ambao wametuwezesha kufanikisha mradi huu.