Ndanda

Kuwasili kwa Mashine CT Scan

Mnamo tarehe 17.8.2021 mashine yetu ya CT Scan imewasili Ndanda.
Ushushaji ulifanywa siku iliyofuata, vifaa viliamishiwa idara yetu ya mionzi.
Ufungaji utachukua wiki moja na mafunzo kwa wafanyakazi wetu utachukua wiki mbili.
Kwa hiyo tunatarajia kuanza huduma kwa wagonjwa wetu mapema mwezi wa tisa.

Upatikanaji wa CT Scan ni hatua muhimu katika maendeleo ya taasisi yetu na faida kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara, Lindi na Ruvuma pia kwa wakazi wa Msumbiji kaskazini.