Kitengo cha wagonjwa mahututi kina vitanda vinne na vifaa vya kisasa. Vitanda vyote vina mfumo wa bomba la oksijeni kutoka kwenye chanzo cha uzalishaji. Tuna vifaa vifuatavyo, mashine tatu za upumuaji,mashine moja ya uchujaji damu,mashine ya kupima moyo, mashine ya utrasound,defibrillator,perfusors,pampu za infusion na zinginezo. Kitengo hiki kina daktari 1 na wauguzi 6, mmoja kati yao anasifa ya utoaji dawa za usingizi. Wagonjwa wodini wanaonwa na wataalamu na mkuu wa kitengo husika.
Mwaka 2021 wagonjwa 244 walipata matibabu kwenye kitengo hiki,na wengi wao wasingepona bila uwepo wa huduma hii maalum ya wagonjwa mahututi. Wagonjwa wamefaidika na huduma hii ya mashine ya upumuaji hasa wakati wa wimbi la pili na tatu la wagonjwa walio na uviko 19. Kwa wagonjwa wenye shida ya figo kutofanyakazi,uchujaji wa damu unatolewa kwenye kitengo hiki.Baadhi ya wafanyakazi wetu wamepata mafunzo ya wagonjwa mahututi katika hospitali ya Taifa Muhimbili na wafanyakazi wote pia wamepata mafunzo na wataalamu waandamizi kutoka Ujerumani.