Ndanda

Makabidhiano ya idara ya Dharura

Mnamo tarehe 10 Mwezi wa tatu 2023 makabidhiano ya jengo lililo ongezwa na kufanyiwa ukarabati wa kina ulifanyika. Ukarabati huu mkubwa ulikusudiwa kuwepo kwa Idara ya dharura na uboreshaji wa idara ya wagonjwa wa nje ya awali, vyumba vya wataalamu mbalimbali, licha ya kuwa na mwonekano wa kuvutia ndani na nje ya jengo kwa upande wa idara ya dharura pia kuna ghorofa ya kwanza yenye ofisi za utawala. Wafanyakazi wetu wanawashukuru sana wafadhili wetu kwa msaada wao mkubwa kwa mradi huu ambao utaleta ubora wa huduma kwa zaidi ya wagonjwa elfu themanini kwa mwaka.     

Wakati unaingia ndani ya Jengo lililokarabatiwa kuna dawati la kutoa maelekezo au maulizo,  pia kuna sehemu ya uchunguzi wa vipimo vya awali muhimu.  Ndani ya Idara ya dharura kuna vyumba vya ufufuo, chumba cha upasuaji wa dharura na vyumba vya kutibu.  Wagonjwa wengine wataingia Idara ya wagonjwa wa nje kwa kuanza na usajiri, huduma ya vipimo vya awali muhimu, kuonana na daktari na kliniki maalum. Katika jengo hili mpya,tunatarajia kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa dharura kwa kutoa kipaumbele kwa wagonjwa kulingana na hali ya mgonjwa. Pia kuepuka mzunguko usio wa lazima kwa wagonjwa wa huduma za nje na jamaa zao kwa kutoa matibabu kwa utaratibu, kitaalamu na muda mfupi wa kusubiri kupata huduma.