Ndanda

Wataalamu Wakuu

Mwezi wa tatu mwaka 2021, wataalamu waandamizi kadhaa kutoka Ujerumani, wamefanya kazi katika kituo chetu. Mtaalamu mmoja  wa usingizi na wagonjwa mahututi. Mmoja muuguzi wa endoscope na mmoja muuguzi wa kitengo cha wagonjwa mahututi. Wamefanya mafunzo ya kitaalamu kwa wafanyakazi wetu katika eneo la uingizaji hewa bandia,  endoscope, ultrasound.

Mbinu mpya na taratibu zimetekelezwa kama upanuzi wa pembeni mwa tundu la koo, upandikizaji wa pacemaker, kutoboa tumbo na kuvuta marongo ya mfupa. Pia wameleta vifaa maalumu vya kisasa kama bronchoscope moja, pacemaker moja na vifaa maalumu kwa ajili ya pericardial paracentesis kwa taratibu za endoscopy na nyinginezo.