Ndanda

Uzinduzi wa NICU

Tangu tarehe 30 Desemba, 2020, kitengo cha watoto wachanga (NICU) inatumika kuokoa maisha ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati na watoto wengine ambao wanahitaji ufuatiliaji mkubwa.
NICU iko katika jengo moja kama vitengo vyetu vipya vya magonjwa mahututi na uchujaji wa mafigo, karibu na wodi wa kuzalia na chumba cha upasuaji.
Tarehe 11, Januari 2021, tulikuwa na sherehe ndogo ya uzinduzi.

NICU ina vifaa na machine ya kisasa.
Incubators mbili zinatumika kwa watoto walio na uzito wa chini sana wakati wa kuzaliwa, pamoja na machine mbili zinazodhibiti joto la mtoto kwa njia ya elektroniki. Hewa ya oksijeni na hewa iliyofinywa inapatikana pamoja na uingizaji hewa kwa watoto kupitia Baby-CPAP.
Mashine mbili za phototherapy ziko tayari kwa watoto wadogo wenye ugonjwa wa manjano.