Ndanda

Utakatishaji wa figo

Kutoka mwezi Oktoba,15th 2018 hadi Oktoba,19th,Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo (nephrologist) Dkt.Kajiru Kilonzo akiambatana pamoja na Nesi Mtaalamu wa usafishaji wa figo Bi Willina Sarina walitembelea Ndanda kwa lengo la kuanzisha huduma ya usafishaji wa figo Dialysis (PD).

Sambamba na hilo mafunzo yalitolewa kwa madaktari na manesi wetu,Hapa wagonjwa watatu walipatiwa huduma za usafishaji wa figo.Huduma hizo zote zilitolewa bure kwa wagonjwa hao.

Ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kabisa kwa huduma hii ya usafishaji wa figo kutolewa Kusini mwa Tanzania!

Mgonjwa wetu wa kwanza Dominik mwenye miaka 22 amefanikiwa kuwekewa figo katika hospital ya taifa ya Muhimbili baada ya kupatiwa usafishaji wa figo katika hospitali yetu na kwa sasa anaendelea vizuri na ameanza mafunzo ya ufundi cherehani katika kiwanda kilichopo Ndanda workshop.

Kwa sasa huduma hii inaendelea kutolewa hapa Hospitalini kwetu kwa wale wanaomudu malipo, na kwa kiasi Fulani hivi Hospitali inachangia gharama.

Hata hivyo wagonjwa saba 7 wameshapatiwa huduma ya PD (June 2020).