Mnamo mwezi Septemba na Novemba mwaka 2021,kambi mbili za magonjwa ya mfumo wa chakula zinafanyika katika hospitali yetu. Kuanzia tarehe 15 Septemba hadi tarehe 8 Octoba,Madaktari bingwa wa mfumo wa chakula kutoka Munich wametutembelea. Wameanzisha ERCP kwenye kituo chetu na huduma tatu zimefanyika kwa mafanikio. Pia wamefanya uchunguzi wa magonjwa ya tumbo na utumbo mkubwa kwa uingiliaji kati kama sindano ya adrenalini,kukatwa na kufunga. Mafunzo ya kina yametolewa kwa madaktari na wauguzi wetu.