Ndanda

Ugonjwa wa korona

Kutokana na mlipuko na kuenea kwa kasi kwa janga la virusi vya COVID 19 maandalizi ya kukabiliana na ugonjwa wa korona yamefanyika kwa kushirikianana na serikali.

Wodi maalum yenye vitanda 11 iliandaliwa pamoja na mavazi pia.

Wafanyakazi wote walipatiwa mafunzo jinsi ya kujikinga na kundi maalum liliundwa akiwemo mtaalamu wa epidemiologia,Mtaalamu wa Mahabara,Daktari (MD)na Afisa msimamizi wa ubora wa Afya.

Uongozi wa hospitali umeanzisha mtambo wa uzalishaji wa hewa ya oksijeni ambayo itatumika kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ICU na chumba cha watoto wachanga NICU,chumba cha upasuaji,chumba cha uzazi.Na hii itatuwezesha kuhudumia vyema vyumba vitatu 3 vya ICU mpya.