Takwimu zinaonyesha hali ya kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake nchini Tanzania ni watu 51 kwa kila watu 100,000 kwa mwaka.Vifo kwa Dunia nzima ni takribani 250,000 kwa mwaka,Asilimia zipatazo tisini (90%) ni kutoka katika nchi zinazoendelea.Kwa sasa karibu nchi nyingi zinazoendelea hazina mpango mkakati wa njia za kujikinga na hivyo kuwa katika hatari kubwa ya ugonjwa huu na kushindwa kukabiliananao.Japokuwa kansa ya kizazi inaweza kuepukika kwa kufanya uchunguzi wa mara kwa mara.
Katika mwezi wa kumi 2019,timu ya daktari mmoja na manesi wawili walihudhuria mafunzo maalum katika Taasisi ya kansa Ocean Road Dar Es Salaam kwa lengo la kuja kuboresha huduma hii katika Hospitali yetu.
Kwa hatua za kujikinga na msingi ,elimu ya afya hutolewa kwa wanawake wote wanaohudhuria hospitalini, kwetu kwa magonjwa ya nje na ndani ya wodi pia.HPV kinga inapatikana kwa wasichana kati ya umri wa miaka 9-14.
Pili tunatoa nafasi ya uchunguzi kila Alhamisi.Njia inayotumika kwa sasa ni uchunguzi kwa kutumia acetic acid (VIA) na Lugol’s Iodine (VILI) na wale wenye umri zaidi ya miaka hamsini > 50 inatumika cervical smear na Papanicolaou (PAP smear).Wote wanaogundulika kuwa na vimelea vya ugonjwa ,hutibiwa kwa cryotherapy.
Uchunguzi ni bure lakin kwa kipimo cha PAP smear wagonjwa hupaswa kuchangia shilingi elfu ishirini (20,000 Tsh).