Shukrani kwa mchango wa ukarimu kutoka Mission Austria, tumefanikiwa kukarabati vyoo vya wodi zetu za matibabu za wanaume na wanawake magonjwa ya mifupa na wanaume magonjwa kawaida. Malengo yalikuwa ni kukarabati vyoo viwe vya kisasa na safi ambavyo havina vizuizi kwa wagonjwa wanaotumia kiti cha magurudumu, waweze kuingia na kutumia vyoo na kuoga. Pia kufunga taa zenye mwanga wa kutosha ili vyoo viweze kutumika wakati wa jioni na usiku.
Ujenzi ulianza mwaka 2021 mwezi wa kumi na moja na makabidhiano yamefanyika mwezi wa pili mwaka 2022. Kila jengo la choo kuna vyoo viwili na bafu mbili ikiwepo choo na bafu kwa wagonjwa walemavu. Milango ya kioo mchanganyiko imewekwa kwa ajili ya faragha. Taa kadhaa zimewekwa pia kwa ajili ya kutoa mwanga wa kutosha.