Ndanda

CT Scan

Makabidhiano ya kituo cha kujaza oksijeni

Tarehe 26.2.2022 mtambo wa kujaza oksigeni uliwasili Ndanda Hospitali. Ufungaji ulianza mara moja na makabidhiano yalifanyika tarehe 4.3.2022. Tumepokea pia mitungi ya oksijeni  30 na oksijeni purity analyzer.
Baada ya kuchelewa kupokea kwa muda mrefu tunashukuru sana vifaa vyote vimepokelewa na kufungwa na mfumo wote unafanya kazi vizuri sana. Sambamba na ufungaji wa kituo cha kujaza oksijeni, mabomba ya oksijeni yameongezwa kuelekea wodi ya watoto na wodi binafsi.

Endapo itatokea kasoro ya kiufundi wa mtambo wa kuzalisha oksijeni itajibadilisha kidijitali na kutumika mitungi ya oksigeni kumi ambayo itahakikisha oksijeni inapatikana kupitia mabomba. Mitungi ya oksijeni ni muhimu sana kwa usafirishaji wa wagonjwa ndani ya hospitali na pia katika kesi ya rufaa. Mitungi hiyo pia itawezesha kusambaza oksijeni kwa vituo vinavyotuzunguka. Kichakata usafi cha oksijeni hupima na kudhibiti kabisa usafi wa oksijeni ambayo utolewa na mtambo wa oksijeni.
Mradi huu umeungwa mkono na kwa ukarimu na MISEREOR kupitia BEGECA na Humatitäre Hilfe Landsberg e.V. Asante sana kwa wote walochangia mradi huu mkubwa!