Ndanda

Kipimo cha Endoscopy

Kwa mwezi Novemba 2018 na mwezi juni, 2019, Dkt Soeren Gatz na Bi,Ottilie Ecke walitutembelea Ndanda kwa lengo la kuanzisha kitengo cha utoaji huduma kwa njia ya video iitwayo Video-Endoscopy katika Hospitali yetu.

Mafunzo kabambe yalifanywa kwa madaktari na manesi wetu pia na madaktari kutoka hospitali zingine zinazotuzunguka.

Hivi sasa,video-egastroscopy,colonoscopy na bronchoscopy vinafanywa kwa kutumia vifaa vya kisasa na vyenye hadhi ya juu.

Mbali na matibabu pia tunatoa huduma za uchunguzi kwa njia ya endoscopy kama vile kupata picha, tunaweza kutibu wagonjwa wanaotapika damu kunakosababishwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo vidonda vya dumbo, kwa kutumia njia ya kuchoma sindano yenye adrenaline au kwa kufunga mishipa na raba bendi ndani ya tumbo.
vilevile kipimo hichi kina uwezo wa kutoa vitu mbalimabli ambavyo huwakwama wagonjwa hasa watoto mfano miiba ya samaki , pesa n.k kutoka katika tumbo

Idadi ya wagonjwa imeongezeka kutoka 12 kwa mwezi ndani ya mwaka 2018 kufikia karibu wagonjwa 50 kwa mwezi 2019 na bado idadi inazidi kukua.

Gharama ya uchunguzi wa tiba ya endoscopy si aghali sana kwa wagonjwa ni Tsh 30,000/= tu.