Ndanda

Upasuaji wa mtoto wa jicho

Kuanzia 20/1/2020 mpaka 8/3/2020,Daktari Bingwa wa macho kutoka Ujerumani Dkt Grasbon,alitutembelea tena Ndanda.

Aliweza kufanya huduma ya upasuaji wa mtoto wa jicho kwa wagonjwa 170, akisaidiwa na waaguzi waandamizi na wafanyakazi wa hospitalini kwetu.

Mgonjwa ilimpasa kulipia gharama ya kiasi cha Tsh 100,000/= tu.Ambayo ni gharama ya upasuaji,kitanda na chakula.

Idadi hii kubwa ya wagonjwa inaonyesha wazi wazi uhitaji mkubwa wa Daktari bingwa wa macho hapa kwetu.

Kwa msaada wa Christoffel Blind Mission, kwa sasa tunamsomesha Daktari mmoja wa macho mwenye elimu ya Shahada ya Uzamili kuhusiana na magonjwa ya macho.(ophthalmology).