Ndanda

Outreach

Mnamo Disemba,2019 mpaka februari 2020 tulitembelea vijiji kadhaa kuchunguza na kutoa elimu ya afya kwa wakaazi wa Ndanda na vijiji vya pembeni.

Timu ya Daktari mmoja na manesi watatu 3 walitembelea vijiji sita 6 navyo ni:Njenga,Mpowora,Liputu,Mwena,Mkalapa na Tuungane.

Watu wote waliohudhuria walichunguzwa shinikizo la damu,na kisukari.Ushauri nasaha na kupima virusi vya Ukimwi (vvu) vilifanyika,vile vile elimu juu ya chanjo ya homa ya ini (Hepatitis B) na Uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake ilitolewa pia.

Kwa ujumla wake watu 747 walihudhuria katika uchunguzi huu. Watu 138 walikutwa na shinikizo la damu,watu 80 kati yao walikuwa ni wagonjwa wapya wa shinikizo la damu. wagonjwa 9 waligundulika na kisukari,6 kati walikuwa wagonjwa wapya. watu 11 walikutwa na virusi (vvu), hao walikuwa wenye maambukizi mapya.

Huduma hizi zote hutolewa bure kwa watu wote.