Ndanda

Chuo cha Uuguzi

Maombi

Fomu za maombi zinaweza kupakuliwa kutoka kwa tovuti, www.ndandahospital.org. au kufanya maombi mtandaoni. Kitengo cha udahili kinashughulikia kufanya upembuzi yakinifu kwa waombaji wote kuangalia wale wenye vigezo stahiki.

1.1 Maombi ya moja kwa moja Chuoni

Mwanafunzi anayetarajiwa hutuma maombi moja kwa moja Chuoni kupitia barua pepe ndandanursing@gmail.com au kuleta moja kwa moja mkononi katika ofisi ya usahili na kufika na vyeti vyote vya kitaalam na vingine vinavyohitajika kwa ajili ya uhakiki.

1.2 Maombi ya Mtandaoni

Mwanafunzi hujaza sehemu zote zinazohitajika kupitia mtandao na kuambatanisha vitu vyote muhimu kwa uthibitisho.

Unaweza kupakua fomu ya maombi hapa: